![]() |
Sheikh Ponda Issa Ponda, Katibu wa Kamati ya Kutetea Haki za Waislamu Tanzania. |
Waislamu nchini Tanzania wamepinga kauli iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dk Albina Chuwa aliyesema kuwa Serikali ya Tanzania haipangi mipango yake ya maendeleo ya wananchi kwa kuangalia itikadi au dini na kabila la mtu, hivyo haiwezi kurejesha kipengee cha dini katika Sensa ya Watu na Makazi.
Aidha Waislamu nchini Tanzania wameelezea kushangazwa kwao na idadi inayotolewa na Kanisa Katoliki kuhusu idadi ya Waislamu Tanzania wakati kipengee cha dini hakipo katika dodoso za Sensa ya Watu na Makazi.Katibu Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda, ambaye pia ni Katibu wa Kamati ya Kutetea Haki za Waislamu Tanzania, amesema kujibu matamshi ya Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Dk. Chuwa kwamba Shura ya Maimamu itahakikisha Waislamu hawashiriki Sensa ya Watu na Makazi iwapo Serikali ya Tanzania haitarudisha kipengele cha dini katika maswali wanayoulizwa wananchi. Amesisitiza kuwa, haoni hoja ya msingi ya kuondoa kipengele cha dini katika sensa, kwani uzoefu unaonesha kuwa, licha ya Serikali kuondoa kipengele hicho, lakini makundi yenye mwelekeo maalumu hutumia nafasi hiyo kutoa takwimu za idadi ya Waislamu, Wakristo na wananchi wenye imani nyingine.
Sheikh Ponda ametoa mfano akisema, mwaka 2008, Wakristo wa Kikatoliki nchini Tanzania walitoa takwimu wakidai kuwa Waislamu ni asilimia 34, Wakristo asilimia 44 na Wapagani asilimia 22 nchini Tanzania na kuhoji takwimu hizo zimetolewa kwa kutegemea kigezo gani wakati kipengee cha dini kimetolewa na Serikali katika sensa?
Katibu Mkuu huyo wa Shura ya Maimamu Tanzania pia amehoji akisema, hivi karibuni pia Televisheni ya Serikali ya Tanzania TBC iliripoti kuwa Waislamu ni asilimia 32, Wakristo asilimia 52 na Wapagani asilimia 16 wakati Idara ya Uhamiaji ikionesha kuwa mwaka 2010 Waislamu walikuwa ni asilimia 35,Wakristo asilimia 32 na Wapagani asilimia 33?
Aidha amesema Chapisho la Serikali la Ramani ya Taifa linaonyesha kuwa
mwaka 2011 Waislamu nchini Tanzania walikuwa asilimia 35, Wakristo asilimia 45 na Wapagani asilimia 20.
Amesema, mambo hayo yote yanawafanya Waislamu nchini Tanzania wakinaike kuwa Sensa ya Watu na Makazi itajibu madai ya muda mrefu ya Waislamu kutaka usawa katika uongozi wa Taifa na mgawanyo wa rasilimali.

No comments:
Post a Comment