Hamdu zote ni za Allah, Mola Mlezi
wa viumbe pia. Na rehema za Allah na salamu Zake zimfikie Mtume Mtukufu
Mwaminifu na Aali zake watoharifu, wateule na masahaba wake wema.
Msimu wa Hija uliojaa rehema na baraka
umewadia na kwa mara nyingine na watu waliofanikiwa kwenda katika miadi
hii iliyojaa nuru, wamo katika kumiminiwa baraka za Mwenyezi Mungu.
Hapa, ninatoa mwito kwenu nyote mahujaji kutumia fursa ya kuwepo mahala
hapa na kuwemo katika wakati huu, kujiimarisha kimaanawi na kimaada.
Hapa, Waislamu wanaume kwa wanawake wanaitikia labeka mlingano wa Mola
wao Mkubwa wa kujipamba kwa sifa na matendo mema; kwa nyoyo na midomo
yao.
Hapa watu wote wanapata fursa ya kufanya mazoezi ya kudumisha udugu, mshikamano na kujiepusha na maasi. Hii ni kambi ya malezi na mafunzo, ni maonyesho ya umoja, adhama na jinsi umma wa Uislamu ulivyokusanya pamoja sura za watu tofauti, ni kambi ya kupambana na shetani na mataghuti. Hapa Mwenyezi Mungu Mwingi wa hekima na Muweza amepafanya kuwa ni mahala ambapo waumini waweze kuona manufaa yao ndani yake. Tutakapofungua macho yetu ya busara na ibra basi ahadi ya mbinguni itaweza kuenea katika maisha yetu yote; ya kila mmoja wetu na ya jamii nzima. Sifa za kipekee za amali za Hija ni kule kuchanganya kwake dunia na Akhera na kuchanganya kwake masuala ya watu binafsi na ya kijamii. Al Kaaba isiyo na doa na iliyotukuka; kutufu miili na nyoyo za watu katika mhimili mmoja madhubuti na wa milele; amali ya Sai (baina ya Safa na Marwa) na kufanya jitihada za mfululizo na za mpangilio mmoja kutoka nukta ya kuanzia hadi nukta ya kuishia; kugura mahujaji wote kuelekea kwenye nyuga za ufufuo za Arafa na Mash'ar na shauku na uhudhurishaji wa moyo katika Mash'ar na maqam hayo adhimu, huleta unyofu na hali mpya, mapambano ya pamoja ya watu wote ya kukabiliana na vielelezo vya shetani, na hatimaye kwa pamoja na kutoka kila mahala na kila rangi na kila namna; wote wanashiriki kwa pamoja katika amali hizo tukufu zilizojaa neema na utukufu na zilizojaa maana na ishara za uongofu. Sifa za kipekee za faradhi hii zimejaa maana na madhumuni.
Hapa watu wote wanapata fursa ya kufanya mazoezi ya kudumisha udugu, mshikamano na kujiepusha na maasi. Hii ni kambi ya malezi na mafunzo, ni maonyesho ya umoja, adhama na jinsi umma wa Uislamu ulivyokusanya pamoja sura za watu tofauti, ni kambi ya kupambana na shetani na mataghuti. Hapa Mwenyezi Mungu Mwingi wa hekima na Muweza amepafanya kuwa ni mahala ambapo waumini waweze kuona manufaa yao ndani yake. Tutakapofungua macho yetu ya busara na ibra basi ahadi ya mbinguni itaweza kuenea katika maisha yetu yote; ya kila mmoja wetu na ya jamii nzima. Sifa za kipekee za amali za Hija ni kule kuchanganya kwake dunia na Akhera na kuchanganya kwake masuala ya watu binafsi na ya kijamii. Al Kaaba isiyo na doa na iliyotukuka; kutufu miili na nyoyo za watu katika mhimili mmoja madhubuti na wa milele; amali ya Sai (baina ya Safa na Marwa) na kufanya jitihada za mfululizo na za mpangilio mmoja kutoka nukta ya kuanzia hadi nukta ya kuishia; kugura mahujaji wote kuelekea kwenye nyuga za ufufuo za Arafa na Mash'ar na shauku na uhudhurishaji wa moyo katika Mash'ar na maqam hayo adhimu, huleta unyofu na hali mpya, mapambano ya pamoja ya watu wote ya kukabiliana na vielelezo vya shetani, na hatimaye kwa pamoja na kutoka kila mahala na kila rangi na kila namna; wote wanashiriki kwa pamoja katika amali hizo tukufu zilizojaa neema na utukufu na zilizojaa maana na ishara za uongofu. Sifa za kipekee za faradhi hii zimejaa maana na madhumuni.
Ni amali kama hii ndiyo ambayo
inauunganisha moyo na kumkumbuka Mwenyezi Mungu, na kuujaza nuru na
kuunawirisha upweke wa moyo wa mwanadamu kwa imani na taqwa na wakati
huo huo kumvua mwanadamu kutokana na mzingiro wa ubinafsi na
kumsahilishia mambo katika jamii iliyopambika kwa sura za kila namna, ya
umma wa Kiislamu na kumvisha nguo ya kujiepusha na madhambi ambayo
huilinda roho yake kutokana na mashambulizi yaliyojaa sumu ya
mashambulizi na vile vile humuongezea nguvu na moyo wa kupambana na
mashetani na mataghuti. Ni mahala hapo ndipo ambapo hujaji anapoweza
kuonana na Waislamu wenzake wengi wanaunda umma mkubwa wa Kiislamu na
kuona kwa karibu nguvu na uwezo wa umma huo na hivyo kupata matumaini
kuhusu mustakbali mwema na vile vile kupata hisia za wajibu wa kutoa
mchango wake wa kuimarisha umma huo na pia kama atapata taufiki na
msaada wa Mwenyezi Mungu aweze kutoa bay'a na kutangaza utiifu wake kwa
Mtume (Muhammad) Mtukufu wa daraja na kufunga mithaki na ahadi imara kwa
Uislamu azizi na kutia nia ya kweli ya kuijenga kiimani nafsi yake,
kuleta marekebisho katika umma na kutia nguvu neno la Uislamu.
Mambo yote haya mawili, yaani kuijenga
nafsi na kuujenga umma (wa Kiislamu) ni faradhi zisizoishiwa na wakati
na wala zisizofungwa. Njia za kuweza kufanikisha faradhi hizo mbili si
nzito kwa watu wenye mazingatio na wanaoangalia mambo kwa kina katika
utekelezaji wa majukumu ya kidini na kutumia vizuri akili, tabasuri na
wenye mtazamo wa mbali.
Kujenga nafsi huanzia kwenye kupambana
na hisia za kishetani na kufanya juhudi za kujiepusha na madhambi na
kujenga umma huingia sura kwa kumjua adui na njama zake, kufanya
jitihada za kupelekea mashambulizi, hadaa na uadui wa maadui usiwe na
athari zozote na hadi kufikia kwenye kuziunganisha nyoyo na mikono
pamoja na lugha za matabaka yote ya Waislamu na mataifa yote ya
Kiislamu.
Katika wakati huu tulio nao hivi sasa,
moja ya masuala muhimu zaidi ya umma wa Kiislamu ambalo lina mfungamano
(wa moja kwa moja) na mustakbali wa umma wa Kiislamu, ni matukio ya
mapinduzi katika nchi za kaskazini mwa Afrika na katika eneo la
Mashariki ya Kati ambayo hadi sasa yameshapelekea kuanguka tawala kadhaa
fasidi na vibaraka wa Marekani na waitifaki za Uzayuni na kuzitikisa
tawala nyingine kama hizo. Kama Waislamu watapoteza fursa hii adhimu na
iwapo watashindwa kutumia fursa hii katika kuujenga vizuri na kuleta
marekebisho kwenye umma wa Kiislamu, basi watakuwa wamepata hasara
kubwa. Hivi sasa mabeberu wavamizi na waingiliaji wa masuala ya ndani ya
mataifa mengine wanafanya juhudi zao zote kujaribu kupotosha harakati
hizo adhimu za Kiislamu.
Katika harakati hizo kubwa, Waislamu
wake kwa waume wamesimama kupambana na ukandamizaji wa watawala (wao
madhalimu) na kupambana na udhibiti wa Marekani ambao umepelekea
kudhalilishwa na kudunishwa mataifa ya Waislamu na kusababisha
kushuhudiwa ushirikiano baina ya tawala za nchi hizo na utawala mtenda
jinai wa Kizayuni. Waislamu wamegundua kuwa kitu kinachoweza kuwaokoa
katika mapambano haya ya kufa na kupona ni Uislamu, mafundisho ya dini
hiyo tukufu na nara na kaulimbiu zake zenye uwokovu na hilo
wamelitangaza wazi wazi. Ajenda yao kuu wameifanya kuwa ni kulitetea
taifa madhulumu la Palestina na kupambana na utawala ghasibu (wa
Kizayuni). Wamenyoosha mkono wa urafiki kwa mataifa yote ya Waislamu na
wanataka kuona umma wa Kiislamu unashikamana na kuwa kitu kimoja.
Hii ndiyo misingi mikuu ya harakati za
wananchi kwenye nchi ambazo katika kipindi cha miaka miwili iliyopita,
wananchi wake wamenyanyua bendera ya uhuru na mabadiliko na kujitokeza
kwa viwiliwili na roho zao kwenye medani za mapinduzi na ni mambo kama
haya ndiyo yanayoweza kuwa misingi mikuu ya kuleta marekebisho katika
umma mkubwa wa Kiislamu. Kusimama imara na kushikamana vilivyo na
misingi mikuu ni sharti la lazima la kuweza kupata ushindi wa mwisho wa
harakati za wananchi kwenye nchi hizo.
Lengo la adui ni kutaka kuhakikisha
anateteresha misingi hii mikuu. Mikono fasidi ya Marekani na NATO na
Uzayuni inatumia baadhi ya mighafala na mitazamo finyu kujaribu
kupotosha wimbi la harakati ya vijana Waislamu na wanatumia jina la
Uislamu kuwagombanisha Waislamu na wanaiita jihadi ya kupambana na
ukoloni na Uzayuni kuwa ni ugaidi usio na macho katika ulimwengu wa
Kiislamu ili Waislamu wauane wao kwa wao na hivyo maadui hao wa Uislamu
waweze kuokoka na Uislamu na wanajihadi wake watazamwe kwa sura mbaya na
chafu.
Baada ya maadui kukata tamaa kwa kuona
kuwa hawawezi kuushinda Uislamu wala kuzima nara na kaulimbiu zake, hivi
sasa wameamua kuzusha fitna kati ya makundi tofauti ya Waislamu na
wanafanya njama za kueneza chuki dhidi ya Ushia na chuki dhidi ya Usuni
ili kuzuia kupatikana mshikamano na umoja katika umma wa Kiislamu.
Maadui wanawatumia vibaraka wao katika
eneo (la Mashariki ya Kati), kuzusha mgogoro nchini Syria ili
kuzishughulisha akili za mataifa ya dunia na kuzifanya zisahau masuala
muhimu ya nchi zao na zisahau pia hatari zinazowakabili. Maadui hao
wanajaribu kuwashughulisha (Waislamu) na masuala ya umwagaji wa damu
ambayo maadui wameyazusha wao wenyewe. Vita vya ndani nchini Syria na
kuuliwa vijana wa Kiislamu kwa mikono ya Waislamu wenzao ni jinai ambazo
zilianzishwa na Marekani na Uzayuni na tawala tiifu kwa maadui ambazo
wanazidi kuchochea moto huo. Nani anaweza kuamini kuwa, tawala ambazo
zilikuwa waungaji mkono wa madikteta waovu wa Misri na Tunisia na Libya,
hivi sasa wamekuwa waungaji mkono wa kutaka demokrasia taifa la Syria?
Kadhia ya Syria ni suala la kulipiza kisasi dhidi ya utawala wa nchi
hiyo ambao katika kipindi cha miongo mitatu ulikuwa umesimama peke yake
kupambana na Wazayuni maghasibu na kuyaunga mkono makundi ya
wanamuqawama wa Palestina na Lebanon.
Sisi tunaliunga mkono taifa la Syria na
tunapinga uchochezi na uingiliaji wa aina yoyote ile wa kigeni nchini
humo. Marekebisho ya aina yoyote ile nchini humo inabidi yafanywe na
wananchi wenyewe na kwa kutumia njia zinazokubaliwa kikamilifu na
wananchi wa taifa hilo. Hatua ya mabeberu wa kimataifa ambao kwa msaada
wa tawala za vibaraka wao katika eneo hili wanatumia kisingizio cha
kuenea mgogoro na wakati huo huo kutumia kisingizio cha kuweko mgogoro
kuhalalisha kufanya kila aina ya jinai nchini humo ni hatari kubwa
ambayo kama tawala za eneo hili hazitajiepusha nayo basi inabidi
zisubiri zamu yao ifike ya kukumbwa na hadaa hizo za kibeberu.
Makaka na madada! Msimu wa Hija ni fursa
ya kutaamali na kuyaangalia kwa kina masuala muhimu ya ulimwengu wa
Kiislamu. Hatima ya mapinduzi ya eneo hili na juhudi za madola makubwa
yaliyojeruhiwa kutokana na mapinduzi (ya wananchi wa eneo hili) za
kutaka kuyapotosha mapinduzi hayo ni miongoni mwa masuala hayo (muhimu
ya ulimwengu wa Kiislamu ambayo inabidi kuyaangalia kwa kina). Njama za
wasaliti za kutaka kuzusha hitilafu kati ya Waislamu na kuleta ugomvi na
suutafahumu kati ya nchi ambazo zimeamua kushirikiana na Jamhuri ya
Kiislamu; kadhia ya Palestina na juhudi za kuifanya itengwe na kuizima
jihadi ya Wapalestina; propaganda za kueneza chuki dhidi ya Uislamu
zinazofanywa na tawala za Magharibi na uungaji mkono wa tawala hizo kwa
watu wanaomvunjia heshima Mtume Muhammad SAW; kuandaa mazingira ya
kuzuka vita vya ndani na kugawanywa vipande vipande baadhi ya nchi za
Waislamu; kuzitisha tawala na wananchi wa nchi za Kiislamu zilizofanya
mapinduzi kuhusiana na hatari za kupinga siasa za kibeberu za Magharibi
na kueneza dhana potofu kuwa mustakbali wao unategemea kujisalimisha
kwao mbele na madola ya kibeberu na masuala mengine muhimu sana kama
hayo, ni miongoni mwa kadhia muhimu ambazo inabidi ziangaliwe kwa
taamuli na kwa mazingatio makubwa katika fursa inayopatikana kwenye Hija
na chini ya kivuli ya kupendana na kuwa na fikra moja nyinyi mahujaji.
Ni jambo lisilo na shaka kwamba uongofu
na msaada wa Mwenyezi Mungu utawaangazia njia za salama na amani waumini
wenye kufanya jitihada katika mambo yao, والذين جاهدوا فينا لنهدينهم
سبلنا Na wanaofanya juhudi kwa ajili Yetu, Sisi tutawaongoa kwenye njia
Zetu. (al Ankabut - 29:69).
Wassalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh.
Sayyid Ali Khamenei,
30/Mehr/1391 (Hijria Shamsia) inayosadifiana na tarehe tano Dhulhijjah 1433 Hijria.
No comments:
Post a Comment